Housekeeping

Shamool Hotel · Dar es Salaam · Closes 2026-11-29

Kaziplat summary

TUNAAJIRI! Mhudumu wa Usafi wa Hoteli (Housekeeping) Shamool Hotel – Sinza, Dar es Salaam Tunatafuta mfanyakazi mwenye uzoefu wa usafi wa hoteli, anayejituma, mwaminifu na makini katika kazi. Majukumu: • Kusafisha na kuandaa vyumba vya wageni kwa viwango vya juu. • Kuhakikisha usafi wa vyumba, bafu na maeneo ya pamoja. • Kusaidia kazi za laundry, kufua, kupiga pasi na kupanga mashuka. • Kusaidia huduma za wageni na idara nyingine inapohitajika. • Kufanya kazi kwa kujitegemea na kushirikiana na timu. Sifa Tunazohitaji: • Uzoefu wa kazi ya housekeeping hotelini. • Uzoefu wa laundry na kusaidia idara nyingine ni faida. • Umakini, uaminifu, bidii na nidhamu ya kazi. • Kujiongeza — kuona kazi inayohitajika na kuifanya bila kusubiri kuambiwa. • Moyo wa ushirikiano na utayari wa kujifunza kazi mbalimbali. • Kujua Kiingereza ni faida, lakini si lazima (English preferred, not required). Kutuma Maombi: Tuma CV yako, uzoefu wa kazi, mshahara unaotarajia kwa mwezi, na tarehe unayoweza kuanza kazi kupitia: info@shamal.com Nafasi: Housekeeping – Shamool Hotel

View the original advert

See all jobs